Watanzania mjini Roma, jana jioni walikutuna tena kwenye ukumbi wa restaurant ya Wahindi iliyopo kwenye mtaa wa Principe Amedeo kwa ajiri ya kuendelea kuchangisha hela kwaajiri ya misiba miwili ya Watanzania iliyokea siku chache zilizopia. Kikao kiliudhuliwa na watanzania wengi sana. Jumuiya ya Watanzania Roma ambayo ndio inasimamia mikuano hii ya msiba, imefurahishwa sana kuona watu wameitikia wito na kujumuika kwa wingi kwenye kikao hichi. Kikao kijacho kitakuwa siku ya Jumatano tarehe 15 Januari. Mkutano utafanyikia kwenye restaurant ya kihindi kuanzia saa kumi jioni! tunazidi kuwaomba wale wote ambao bado kuchanga wafike ili waweze nao kuchanga.
Hapa Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Ndugu Andrew Chole Mhella akitoa maelezo juu ya maendeleo ya shughuli nzima ya Msiba wa Watanzania Italy. |
Watanzania wakimsikiliza mwenyekiti akielezea jambo. |
Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma |
Mwenyekiti akisisitiza Jambo |
No comments:
Post a Comment