Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Thursday, June 16, 2016

Sunday, May 29, 2016

ANNUAL AFRICAN DAY CELEBRATIONS IN ROME 25 MAY 2016

THE CAKE


TANZANIAN TABLE

Sunday, March 6, 2016

MATOKEO YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA


Jana, jumamosi tarehe 05-03-2016, Watanzania waishio mjini Roma waliokutana kwaajiri ya kuchagua viongozi wapya watakao ongoza jumuiya ya Watanzania Roma kwa kipindi cha miaka miwili.
Nafasi zilizokuwa zinapigiwa kura ni za Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Wajumbe wawili wa Kamati ya kuu ya utendaji.

Matokeo ni kama yafuatavyo:
1. Mwenyekiti - Ndugu Andrew Chole Mhella alishinda kwa

    asilimia 90.


2. Katibu - Ndugu Sammy Kibwana alishinda kwa asilimia 55.


3. Mweka Hazina - Bi. Lilian Mashishi Luhende alishinda kwa
    asilimia 80.


4. Wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji - Ndugu Kondela
     Buhire na Ndugu Bedui Issa.

Kwa niaba ya viongozi wenzangu tunapenda kuwashukuru wasimamizi wa uchaguzi, ndugu Raymond na ndugu Yohana Shija Masalu kwa kusimamia vizuri zoezi zima la uchaguzi.
Tunapenda kuwafahamisha Watanzania wote wa Roma kuwa Katiba na mafomu ya kujiunga na Jumuiya yapo tayari kwa wale ambao bado hawajapata nafasi ya kuyachukua watuinbox tuweze kuwafahamisha namna ya kuyapata mafomu na pamoja na katiba.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.Andrew Chole Mhella
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma.

Sunday, February 28, 2016

TAARIFA MUHIMU: UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA

TAARIFA MUHIMU KWA WATANZANIA ROMA: UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA KUFANYIKA TAREHE 5 MACHI 2016Baada ya Mikutano mitano ya majadiliano, uchunguzi na ukarabati wa Katiba ya Jumuiya ya Watanzania Roma, Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma unayofuraha kuwafahamisha kuwa jana tarehe 20 Februari 2016 zoezi zima la urekebishaji wa katiba ulikamilika. Wajumbe kwa pamoja walipanga tarehe 5 Machi 2016, saa kumi na moja jioni ndio kuwa siku ya uchaguzi wa viogozi wapya. Uchaguzi utaf...anyika kwenye Indian Restaurant via Principe Amedeo 70 (termini). Kwa wale wanaotaka kuchukua mafomu ya kujiunga na Jumuiya tafadhali wasilianane na Katibu (Andrew Chole Mhella - kwa kupitia Inbox). Nafasi za kugombea ni za Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji. Kwa yeyote atakayetaka kushiriki kwenye uchaguzi atatakiwa kujaza na kukabidhi fomu kwenye uongozi unaomaliza muda wake.
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia page hii ya Jumuiya.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki jumuiya ya Watanzania Roma.
Katibu,
Andrew Chole Mhella.

Tuesday, January 26, 2016

NAFASI YA AGIRA KWA DIASPORA KATIKA HOSPITALI YA AGAKHAN DAR-ES-SALAAM

Tunapenda kuwafahamisha wana diaspora kuwa, Hospitali ya Agakhan ina mahitaji ya haraka sana ya wataalamu wa Afya kuziba nafasi mbalimbali za kitabibu zilizo wazi katika hospitali hiyo. Hospitali hiyo imetoa kipaumbele kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kujaza nafasi hizo, baada ya kukosekana kwa wataalam wa kutoka nchini Tanzania. 
Tafadhali wafahamisheni watanzania walioko katika eneo lenu waombe nafasi hizo kwa wingi ili kujaza nafasi husika kama zilivyoainishwa kwenye Tangazo la Ajira lililoambatishwa. Maombi hayo yatumwe kabla ya tarehe 6 Februari 2016, kupitia barua pepe ifuatayo: mary.mlay@akhst.org, nakala kwa diaspora@nie.go.tz, na info@embassyoftanzaniarome.info.


Friday, January 1, 2016

Sunday, December 6, 2015

TAARIFA MUHIMU: KUAGWA KWA MWILI WA MAREHEMU THOMAS RYNOS PETER


UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA UNAPENDA KUWAFAHAMISHENI KUWA, MWILI WA MAREHEMU THOMAS RYNOS PETER A.K.A KIGADI, UTAAGWA KESHO ASUBUHI, TAREHE 07/12/2015 KWENYE MORTUARY YA POLICLINICO UMBERTO I KUANZIA SAA NNE MPAKA SAA TANO NA NUSU ASUBUHI. BAADA YA HAPO TUTAKUTANA KWENYE UKUMBI ULIOPO MTAA WA VIA MAGENTA 53 KUANZIA SAA SABA MPAKA SAA KUMI KWAAJIRI YA SADAKA NA KUOMBOLEZA. MWILI WA MAREHEMU UTAONDOKA SIKU YA JUMANNE TAREHE 08/12/2015 NA TURKISH AIR KWENDA TANZANIA KWAAJIRI YA MAZISHI. KWA NIABA YA JUMUIYA ZOTE ZA WATANZANIA ITALY TUNAPENDA KUWASHUKURU WALE WOTE MLIOKUWA MSTALI WA MBELE KWENYE SAFARI NZIMA YA MAANDALIZI YA KUMSAFIRISHA NDUGU YETU KIGADI.


TUNAOMBA TU WALE AMBAO BADO HAWAJAKAMILISHA MICHANGO YAO WAJE NAYO KESHO MOJA KWA MOJA KWENYE ENEO LA TUKIO.
ASANTENI SANA.


Katibu,
Andrew Chole Mhella

Monday, November 23, 2015

TAARIFA YA MSIBA MJINI ROME

UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA, UNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU THOMAS RYNOS PETER a.k.a KIGADI, KILICHOTOKEA MJINI ROMA JUMAMOSI JIONI TAREHE 21-11-2015. MAREHEMU ALIZALIWA MJINI TANGA 09-06-1962.

MAREHEMU ATAKUMBUKWA NA WENGI KWA UCHESHI NA UPENDO.

ILI TUWEZE KUFANIKISHA ZOEZI ZIMA LA KUUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KWENDA TANZANIA KWAAJIRI YA MAZISHI KAMA TULIVYOOMBWA NA NDUGU ZAKE WALIOPO TANGA, TANZANIA, SIKU YA KESHO JUMANNE TAREHE 24-11-2015, KUANZIA SAA KUMI JIONI KWENYE RESTAURTANT YA KIHINDI ILIYOPO VIA PRINCIPE AMEDEO, MAENEO YA TERMINI, KUTAKUWA NA MKUTANO WA KUCHANGISHA FEDHA.

TUNAOMBA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI MFIKE KWA WINGI ILIZOEZI ILI TULIKAMILISHE MAPENMA IWEZEKANAVYO.

UPATAPO UJUMBE HUU TAFADHALI MFAHAMISHE NA MWENZIO.

MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI MR. KIGADI, AMEN.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

KATIBU,
JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA

Tuesday, November 17, 2015

TANZANIA MAINLAND INDEPENDENCE DAY CELEBRATIONS IN ROME: MAANDALIZI YAMEANZA MUDOGO MDOGO. MNAOMBWA MUUDHULIE MIKUTANO YA JUMUIYA ZENU MUWEZE KUELEZWA MIPANGILIO YA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA UHURU 2015. KWA UPANDE WA ROMA KUTAKUWA NA MKUTANO SIKU YA JUMAMOS TAREHE 21 NOVEMBER 2015 PALE INDIAN RESTAURANT (VIA PRINCIPE AMEDEO) TERMINI AREA, KUANZIA SAA TISA JIONI. NYOTE MNAKARIBISHWA KWA WINGI.