Jumuiya ya Watanzania Roma imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba kutoka Napoli za ndugu JUMANNE MOHAMED MKASI ajulikanaye na wengi kama "TUESDAY". Marehemu Tuesday, ambaye alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu alifariki jana asubuhi tarehe 15/11/2017 hospitalini mjini Napoli alipokuwa amelazwa kwaajiri ya matibabu. Marehemu kwa Tanzania ni mkazi wa kata ya Manzese, Mtaa wa Mnazi Moja mjini Dar -es -Salaam.
Uongozi wa Jumuiya unapenda kuwafahamisha watanzania mjiini Roma kuwa jumamosi ya tarehe 18 November 2017, kuanzia saa kumi jioni, kutakuwa na mkutano wa kuchangisha fedha kwaajiri ya kuhusafirisha mwili wa marehemu kwaajiri ya mazishi nchini Tanzania. Mkutano utafanyika kwenye mtaa wa Via Principe Amedeo 70 (Indian Restaurant) maeneo ya Termini Station.
Kwa wale mtakaoshindwa kufika siku ya Jumamosi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wenu, mnaombwa muwasiliane na Mwenyekiti, Andrew Chole Mhella, Ndugu Kondela Buhire au ndugu Mwishehe kwaajiri ya michango yenu.
Upatapo ujumbe huu tafadhali unaombwa umfahamishe na mwenzako.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu "Tuesday" mahali pepa peponi. Amen.
Mwenyekiti,
Andrew Chole Mhella
Andrew Chole Mhella
CBD oil Hong Kong
ReplyDeleteRick Simpson oil Hong Kong
Ricks hemp oil Hong Kong
Medical cannabis Hong Kong
Hemp oil Hong Kong
Where to buy CBD oil
CBD Hemp oil Hong Kong
Rick Cannabinoild oil Hong Kong
Cannabidiol Hong Kong
Rick Cannabinoild Hong Kong