Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Monday, June 24, 2013

BALOZI WILFRED NGIRWA AANZA RASMI UENYEKITI WA BARAZA LA FAO



Pichani anaonekana Balozi Ngirwa akiendesha Mkutano wa 147 wa Baraza la FAO uliofunguliwa leo asubuhi. Pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Baraza na Mkutano Mkuu wa FAO.

Leo asubuhi Balozi Wilfred Joseph Ngirwa amepokelewa kwa shangwe na bashasha alipoketi rasmi, kwa mara ya kwanza, kwenye kiti chake tayari kufungua na  kuendesha Kikao cha 147 cha Baraza la FAO.
Balozi Ngirwa alianza kwa kuwashukuru wanachama wote wa FAO kwa kumchagua kwa asilimia 95 kwenye Mkutano Mkuu wa 38 wa FAO hapo tarehe 21 Juni, 2013 na baadaye kumteua rasmi kwenye nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Baraza la FAO (Independent Chairperson of the FAO Council) hapo tarehe 22 Juni, 2013 kama taratibu na kanuni zinavyotaka.
Balozi Ngirwa aliahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uaminifu na kujituma, akiweka mbele maslahi na malengo ya FAO. Aidha, Balozi Ngirwa aliomba ushirikiano kutoka kwa Anathema wa Baraza, na nchi wanachama wote wa FAO kwa ujumla.
Katika mahojiano yetu awali, Balozi Ngirwa alimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa imani kwake na hata kukubali Tanzania impendekeze, kama kanuni zinavyotaka, kama mgombea wa nafasi hiyo. Aidha, alimshukuru kwa dhati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Ben Membe (MP), na Wizara yake kwa ujumla, kwa kampeni nzuri na za mafanikio makubwa. Pia alimshukuru sana Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Eng. Christopher K. Chiza (MP), pamoja na Wizara yake kwa juhudi za hali na mali hadi kupatikana kwa ushindi. Pamoja na shukrani kwa wengine wengi, Balozi Ngirwa alimshukuru Balozi na Watumishi wote wa Ubalozi wa Tanzania Roma kwa  kujitolea kwa dhati kufanya kampeni pevu katika anga za kidiplomasia kwa kipindi chote cha miezi 14 tangu jina lake lilipopendekezwa kwa mara ya kwanza katika duru za FAO na kufungua mlango wa kuungwa mkono na makundi yote, kuanzia na kundi la Africa (FAO Regional Group for Africa) kwenye Mkutano uliofanyika huko Congo-Brazzaville mwezi April, 2012. Aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ubalozi katika kipindi chote cha uwepo wake kwenye nafasi hiyo, pia akitegemea ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania Roma kumwezesha kutekeleza vyema majukumu yake.
Balozi Ngirwa anakuwa mwafrika wa pili kuchukua nafasi hiyo tangu mwaka 1945 wakati lilipoanzishwa Shirika hili la Chakula la Umoja wa Mataifa. Balozi Ngirwa, mtaalam wa masuala ya kilimo na chakula, ana uzoefu mkubwa kupitia utumishi wake uliomfikisha hadi ngazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Tanzania. Baadaye aliteuliwa na Mhe. Rais kuja Roma kama mwakilishi wetu wa kudumu kwenye mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa, ambapo alipata pia uzoefu mkubwa katika diplomasia kwa miaka 6, hadi alipostaafu mwezi Machi, 2012. Ni matumaini yetu kuwa Watanzania tutampa ushirikiano na kumsaidia kuiwezesha Tanzania kufaidika na kuendeleza vyema maslahi yake katika mashirikiano na mashirika haya ya Umoja wa Mataifa jijini Roma.
Tunamtakia Kilahama la heri.


Pichani ni Balozi Eng. Dr. James Alex Msekela akiwa na Mwambata Kilimo na msaidizi wake Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Roma, Bw. Ayoub Mndeme, wakishiriki kwenye kikao cha 147 cha Baraza la FAO leo asubuhi.

Source: Tanzanian Embassy in Italy.

No comments:

Post a Comment