Shirika
la Chakula na Kilimo FAO, Ijumaa katika Kikao chake cha 38,
lilimchangua Balozi Wilfred Joseph Ngirwa, kuwa Mwenyekiti mpya wa
Baraza la FAO, kwa kipindi cha miaka miwili ijayo June 2013 hadi June
2015.
Balozi Wilfred Ngirwa, amechaguliwa kushika nafasi hii ya Mwenyekiti wa kujitegemea wa
Baraza katika maana ya Mwenyekiti aliye huru asiyegemea upande wowote,
kwa shindi wa asilimia 96 kati ya kura zote zilizopigwa na wajumbe wa
Baraza 154, kura za ndio zikiwa 146, kura turufu 7 na kura za hapana 1( moja) .
Balozi
Wilfred Ngirwa alizaliwa Tanzania mwaka 1948 katika familia ya kawaida
ya Watanzania,Bukoba Mkoani Kagera. Ni
mtalaam katika uwanja wa Kilimo na uchumi, kazi aliyoifanya wa muda wa
miaka 38 , ambamo huduma yake ilitambulwia vyema hasa kwa mchango wake
kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Tanzania na katika Mashirika
matatu ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na huduma kwa Mkulima, ambayo
ni Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) Shirika la Mfuko wa Maendeleo
katika Kilimo( IFAD), na Shirika la Mpango wa Chakula (WFP). Na pia
kama Mwakilishi wa Tanzania katika mashirika hayo,uwakilishi uliompa
heshima ya kuwa Balozi.
Katika
Khafla ya kumpongeza Balozi Ngirwa, iliyoandaliwa na Ofisi ya Ubalozi
wa Tanzania nchini Italy, Waziri wa Kilimo Tanzania, Mheshimiwa
Waziri Christopher Kizza , alisema, ushindi wa Balozi Ngirwa katika
kinyanyang’iro cha cheo hicho, umekuwa ni ushindi na heshima kubwa kwa
Afrika, na hususani kwa Watanzania wote. Na hivyo ushindi huu ni
changamoto inayodai hasa tanzania kwa ujumla kuendelea kuishi kwa amani
na utulivu, katika kudumisha heshima ya Tanzania kwenye ngazi za
Kimataifa,
na kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, na hasa Wakulima na wafugaji
vijijini.
Waziri
aliomba ushirikiano wa karibu na Mwenyekiti Mpya wa Baraza la
FAO,akisema, ingawa kwa cheo chake hakifungamani na upande wowote, bado
Afrika inatazamia
kunufaika zaidi na mchango wake, katika kubadili maisha ya mkulima wa
Afrika hasa kwa kutokana na uzoefu wake katika maisha yake ya kawaida ya
mkulima wa Afrika Vijijini.
Na Balozi James Nsekela
, katika hotuba yake fupi kwa Khafla hiii, alionyesha furaha yake
kwamba Kupitia Balozi Ngirwa , Tanzania imeaminiwa kuliongoza Shirika la
FAO. Aliiaja kazi hii kuwa ni nzito na nyeti
yenye kuhitaji weledi na ushirikiano wa karibu na watendaji wengine.
Vivyo katika Khafla hii alikuwepo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Zanzibar, Dr. gharib .
Na
Balozi Ngirwa, alitoa shukurani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya
Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuidhinisha jina lake liwakilishwe
FAO, kama mgombea wa cheo cha Mwenyekiti wa kujitegemea katika Baraza
la FAO. Na pia aliwashukuru wote, waliomtia moyo wa kugombea kiti
hicho. Na
kwamba akiwa katika cheo hiki kipya atafanya kazi zake katika misingi
ya imani yake kwamba , FAO ni shirika ambamo misingi ya maamuzi yake
imesimikwa katika misingi ya makubaliano ya nchi wanachama wa Umoja wa
Mataifa. Na hivyo, mamlaka yake yatazingatia rejea msingi zilizotajwa
katika nyaraka za FAO, na Mpango wa Kidharura wa Utendaji kama
ilivyo ainishwa katika hati za makubaliano za Fao.
Balozi Ngirwa anaanza Kazi yake Mpya Jumatatu 24 June 2013, katika makao makuu ya FAO , Mjini Roma.
Na Mrs. Tabitha Janeth Mhella
BALOZI NGIRWA AKIPONGEZWA NA WAZIRI WA WIZARA YA KILIMO WA TANZANIA MHESHIMIWA CHISTOPHER KIZZA.Na Mrs. Tabitha Janeth Mhella
WAZIRI WA KILIMO TANZANIA
WAKATI UCHAGUZI UKIENDELEA. TOKA KUSHOTO NI MH. BALOZI NGIRWA KATIKATI NI BALOZI WA TANZANIA ITALY MH. JAMES MSEKELA NA KULIA NI WAZIRI WA KILIMO TANZANIA MH. CHRISTOPHER KIZZA.
BALOZI NGIRWA AKIPONGEZWA.
TIMU YA TANZANIA ILIYMSINDIKIZA BALOZI NGIRWA SIKU YA UCHAGUZI.
WAKATI WA CHAKULA CHA USIKU PAMOJA NA MH. BALOZI NGIRWA.
BALOZI NGIRWA AKIPATA PICHA YA PAMOJA WAKATI WA CHAKULA CHA USIKU CHA KUMPONGEZA KILICHOANDALIWA NA MH. BALOZI JAMES MSEKELA.
WAHESHIMIWA WAKIGONGESHA GLASI KUMPONGEZA BALOZI NGIRWA.
KUTOKA KUSHOTO NI KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY NDG. ANDREW CHOLE MHELLA NA KATIBU MSAIDIZI WA JUMUIYA HIYO BI. DIANA PAUL OLOTU.
Picha Zote zimepigwa na Mr. Msemo toka ubalozi wa Tanzania Italy.
No comments:
Post a Comment