Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Sunday, November 25, 2012

MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA WAFANA

Mkutano Mkuu wa kufunga mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome, ambao ulikuwa ukisubiriwa na Watanzania wengi tokea mjini Roma na vitongoji vyake, ulifanyika kama ilivyopangwa saa kumi jioni jumamosi ya tarehe 24 Novemba 2012.  Mkutano ulifanyika kwenye mtaa wa Giovannni Lanza 122, mjini Roma karibia na Kituo cha Metro cha Termini.

Mkutano huu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Roma, uliongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Mh. Leonce Uwandameno.

Kulingana na katiba ya jumuiya ya Watanzania Roma kipengele namba 6.1, mkutano huu ufanyika kila mwisho wa mwaka mwezi wa kumi na moja. Malengo ya mkutano kwa mwaka huu yalikuwa haya;
  • Kujadili mwenendo wa jumuiya kwenye kipindi cha mwaka mzima wa 2012. Yaani mwenendo wa michango, ushirikiano baina ya jumuiya hii ya Roma na Jumuiya zingine za Kitanzania hapa Italy pamoja na Ubalozi wa Tanzania Italy. Wajumbe pia walijadili mafanikio yaliyoonekana kwenye mwaka wa 2012 na pia bila kusahau matatizo mbalimbali yaliyojitokeza na kuyatafuta suluhisho.
  • Wanajumuiya pia walijadili juu ya Utambulisho wa huduma mpya ya BIMA kwa Watanzania waishio Diaspora. Hoja hii ilionekana kuwavutia waudhuliaji wengi ambapo kila mmoja alichangia mawazo tofauti ambapo uongozi wa jumuiya uliwaahidi wanajumbe kuwa utafikisha maoni yao kwa wahusika ili waweze kutoa maelezo zaidi juu ya hii BIMA.
  • Kuwasihi wanajumuiya na watanzania wote kwa ujumla, juu ya umuhimu wa ushiriki wao kwenye kuchangia maoni kwenye mchakato mzima wa kufanikisha ukamilishaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti, Mh. Leonce Uwandameno akisikiliza Hoja kutoka kwa mjumbe huku Katibu wake akiandika maoni ya Wanajumuiya!


Katibu, ndugu Andrew Chole Mhella akielezea mwenendo wa jumuiya kwa mwaka wa 2012.
Wajumbe wengi walikuwepo kwenye mkutano huu.
Kwa nyuma ni Mwenyekiti Msaidizi Mh. Erasmus Pindu Luhoyo, kwa mbele kushoto ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe na Mikutano ndugu Bakari Hizza pamoja na Mjumbe Bi. Lucy M. upande wa kulia.

 Ndugu Mattia akionekana akisikiliza kwa makini hoja ya Mwenyekiti, kwa pembeni ni Mtoto wake Queen.

 

No comments:

Post a Comment