Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Sunday, February 26, 2012

Mkutano wa Jumuiya ya Watanzania Rome Wapendeza Kuliko

Kama ilivyokuwa imepangwa, jana tarehe 25 Feb. 2012 kwenye ukumbi wa ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Rome, ulifanyika mkutano wa Jumuiya ya Watanzania Roma. Mkutano huu ambao ulikuwa uambatane na uchaguzi wa viongozi wapya ulifana sana japo wanajumuiya hai hawakuwa zaidi ya nusu ya Wanajumuiya wote. Kutokana na kutokuwepo kwa wanajumuiya hai zaidi ya nusu, wanajumuiya waliokuwepo kwa pamoja waliamua kuupeleka uchaguzi mbele mpaka mwishoni mwa mwezi wa nne, kutokana na katiba kutoruhusu kufanya uchaguzi pale wanajumuiya wanapokuwa chini ya nusu. Mgeni wa heshima kwenye alikuwa Kaimu Balozi wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy, mh. Salvatory Mbilinyi. Kwenye huu mkutano, wanajumuiya kwa Pamoja walijadili maswala mbalimbali muhimu kama vile, umuhimu wa kushiriki kwenye vikao mbalimbali vya jumuiya, kujitaidi kutoa michango ya jumuiya na mengineyo mengi. Siku chache zijazo, kamati ya utendaji ya jumuiya ya Watanzania Rome, itakaa ili kujadili maandalizi ya sherehe ya muungano wa Tanzania itakayofanyika mwishoni mwa mwezi wa nne. Mara tu kamati ya utendaji itakapo kaa mtajulishwa hatua itakayo fuata.
Hapa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Mh. Leonce Uwandameno (aliyesimama) akifungua mkutano. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya Andrew Chole Mhella na kulia ni Mweka Hazina ndugu Awadhi Suleiman.



Hapa uongozi wa Jumuiya ukimkabidhi Bi.Gunhild Mwakangale kadi tatu za uanajumuiya. Kadi mbili zingine atazifikisha kwa Bi. Alice Maimu na Bi. Hadija Omari Mwakangale. Hawa wote wanaishi Sardegna kusini kwa Italy.
Wajumbe wakilisakata KWAITO.
Kama mnavyoona, wajumbe wakiandaa kitu tumbo yapenda.
Mwenyekiti akipata picha ya pamoja na Wanajumuiya.
Hapa Bi Gunhild akisho some love kwa Mjumbe, Bi. Thanner.
Katibu akiwa pamoja na Yakubu.
Katibu akiwa pamoja na wajume.

No comments:

Post a Comment