Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Thursday, February 9, 2012

TANGAZO: UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA KUFANYIKA 25 FEB. 2012


Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome, unayofuraha kuwajulisheni kuwa siku ya jumamosi tarehe 25 februari 2012 kuanzia saa nane mchana, kutakuwa na mkutano na uchaguzi wa viongozi wapya wa Jumuiya ya Watanzania Rome.Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Rome kwenye mtaa wa Via Cortina d'anpezzo 185. Wanajumuiya hai wote mnaombwa muwasiliane na katibu ndugu Andrew Chole Mhella ili muweze kupata taratibu nzima za Mkutano huu. Mnaweza kumpata katibu kwa e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it. au kwa simu namba 3479094800. Kwa wale ambao wanapenda kuwasilisha majina yao kwaajiri ya kugombea nafasi hizi mnaombwa mtume majina yenu yakiambatanishwa na nafasi ambayo mnataka kugombea kupitia e-mail ya jumuiya hapo juu. Nafasi ni hizi MWENYEKITI, MWENYEKITI MSAIDIZI, KATIBU, KATIBU MSAIDIZI, MWEHA HAZINA NA NAFASI MBILI ZA WAJUMBE.
Uchaguzi utaendeshwa kwa kufuata kanuni za katiba.

Vipengele hivyo ndivyo vitakavyo saidia kupata viongozi wapya:

5.1 Sifa za Viongozi

Ili mwanajumuiya aweze kugombea au kuchaguliwa kuwa mmoja wa

viongozi wa jumuiya, atatakiwa awe na sifa zifuatazo:

a) Mwenye kuishi kihalali hapa Italia;

b) Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai.

c) Awe na uwezo wa kuongoza jumuiya kwa busara;

d) Awe mwaminifu;

e) Wenye kuheshimu na kutunza vifaa mbalimbali vya jumuiya.


5.2 Uchaguzi wa Viongozi

Uchaguzi wa viongozi yaani mwenyekiti, mwenykiti msaidizi, katibu, katibu

msaidizi, mweka hazina na wajumbe wawili, utafanyika kila baada ya miaka

miwili. Lakini pia unaweza kufanyika wakati wowote ambapo mkutano wa

wanajumuiya utaitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba hii.

5.2.1 Baada ya kiongozi mpya kuchaguliwa, kutakuwa na kipindi cha miezi miwili ya

kukabidhi madaraka.

5.3 Uchaguzi wa viongozi utafanyika katika mkutano utakaoudhuriwa na zaidi ya

nusu ya wanajumuiya. Pale ambapo uchaguzi kwa nafasi inayogombewa

unalenga kuwapata washindi zaidi ya mmoja basi washindi watakuwa ni wale

waliopata kura nyingi kuwazidi wengine hadi kupata idadi inayoitajika kwa nafasi

hiyo inayogombewa.


No comments:

Post a Comment