

ROME: Jana jumanne tarehe 25 May 2010, Balozi za nchi za Africa hapa nchini Italia pamoja na raia mbalimbali wa africa na waharikwa tokea nchi zingine nje ya bara la Africa, walijumuika pamoja kuadhimisha siku ya kiafrica mjini Rome kwenye ukumbi uliopo kwenye Via Appia Nuova. Mwaka huu nchi andalizi ni Malawi lakini kutokana na kutokuwa na ubalozi hapa Italy, jukumu la kuandaa hii sherehe lilifanya na Balozi za nchi nyingine za Africa hapa nchini Italia. Itakumbukwa kwamba kila mwaka nchi ambayo ipo kwenye uongozi wa umoja wa Africa (African Union) huwa inasherekea siku ya Kiafrica kwa kufanya sherehe ambazo huwa zinaalika raia wa nchi nyingine kuja kujionea utamaduni wa mwafrica. Utamaduni kwa maana ya mavazi, vyakula, Vinywaji, miziki na vinginevyo. Itakuwa vizuri pia kukumbuka kuwa Tanzania tuliadhimisha siku hii ya kiafrica (African day) miaka mitatu iliyopita kipindi ambacho tulikuwa tukiongoza Umoja wa Africa ambao mwaka Jana ulikuwa chini ya Libya.
Dada Diana unazidi kupendeza
ReplyDeleteTehe tehe tehe!
ReplyDeletewarembo na nyinyi mlipika nini siku hiyoooooooooo nawaaminia dada zangu.
ReplyDeleteSwali zuri sana!!!!uliza tena!!? Ni mimi Mkereketwa wa Blog hii ya Watanzania Roma.
ReplyDelete