
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome unayofuraha kuwafahamisha wanajumuiya wake wote kuwa siku ya jumamos tarehe 26 June 2010, kutakuwa na mkutano wa Jumuiya ya Watanzania Rome. Mkutano huu utakuwa na lengo la kujadili maswala mbalimbali yanayohusu jumuiya na kuwakaribisha wanajumuiya wapya. Muda na mahali uongozi utawajulisha siku za hivi karibuni. Uongozi unawaomba mjipange vizuri ili siku ya mkutano wote muweze kuwepo. Hii yote ni kwaajiri ya kuimarisha jumuiya yetu. Kwa wale wote ambao hamjajiandikisha, mnakumbushwa kuwa jumuiya haibagui mtu yoyote kwa namna yeyote ile, kwa hiyo wote mnakaribishwa kuchukua fomu za kujiandikisha. Of course, hii yote ni baada ya kusoma na kuielewa katiba. Kwa maelezo zaidi mnaombwa muwasiliane na mwenyekiti wa Jumuiya Mh. Leonce Uwandameno au Katibu wa Jumuiya Ndg. Andrew Chole Mhella kwa e-mail hii: watanzaniarome@yahoo.it au kwa namba hii ya simu 3479094800. Asanteni
No comments:
Post a Comment