
Dr. Boniface akielezea kazi yake iliomfanya ale nondoz ya udadtari

Watanzania wakiongozwa na Mh. Balozi W. Ngirwa na ndugu mbalimbali walikuja kushuhudia utetezi huu.
Mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Rome Dr. Boniface J. Mhella jana jioni(24-03-2010) alitetea kazi yake ya udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Pontifical University of St. Thomas of Aquinas "ANGELICUM" na kufanikiwa kuikwaa nondoz ya Udaktari. Dr. Boniface alifanya research kwenye mada hii: COMPLEMENTARY FINANCING FOR POVERTY REDUCTION AND ECONOMIC DEVELOPMENT, with reference to Tanzania (1961-2006). Jumuiya ya Watanzania Rome inapenda kumpongeza Dr. Boniface na kumtakia mafanikio mema.
HONGERA SANA MHESHIMIWA KWA NONDOZ ULIZOKULA... HAYO NDIYO MALENGO SAHIHI YA KUWEPO KWENU UGHAIBUNI YAANI TAFUTENI ELIMU MRUDI NAYO HAPA BONGO ITUSAIDIE SIYO KUFUNGUA MATAWI YA VYAMA VYA SIASA AMBAYO HAYANA TIJA KWA MTANZANIA!
ReplyDeleteHongera sana mazee!! basi tunalusubiri hapa nyumbani uje tujenge nchi hii masikini inayoliwa na wajanja. Usikubali kuwa mwenyekiti wa CUF Napoli, yaani usiwe bendera fata upepo.. rudi tujenge nchi yetu.
ReplyDeleteMdau Kihonda, Mji kasoro bahari.