Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Saturday, December 26, 2009

Ujumbe wa Kufunga Mwaka kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome



Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome, napenda kuwatakieni Watanzania wote muishio Italia na seheme nyingine duniani, Merry Christmas na zaidi kabisa Happy New Year 2010 yenye amani na mafanikio mema kwa kila mmoja wenu. Zimebaki siku chache tu kama mnavyoona hapo juu kwenye count down ya blog yetu. Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Watanzania waishio Rome kwa kushirikiana na uongozi huu kwenye matukio mbali mbali tokea kuanzishwa kwa Jumuiya hii tarehe 4 mwezi wa saba 2009.

Itakumbukwa kuwa Jumuiya yetu ya hapa Rome ilianzishwa tarehe 4 mwezi wa saba 2009 mjini Rome chini ya usimamizi wa mgeni rasmi Mh. Balozi A. Karume. Kwenye Mkutano huo viongozi watatu (Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina) walichaguliwa kuongoza Jumuiya hii.

Itakumbukwa kwenye kipindi cha muda mfupi tokea kuanzishwa Jumuiya yetu tulipata msiba mkubwa wa mwamajumuiya, Mtanzania mwenzetu marehemu Moses Kiumbi aliyefariki dunia kwenye hospitali ya Policlinico Umberto I mjini Rome tarehe 22 oktoba 2009 alipokuwa akitibiwa majeraha makubwa aliyoyapata pale alipodondoka baada ya kushuka kwenye bus tarehe 17 Oktoba 2009. Tulifanikiwa kumuaga marehemu tarehe 30 Oktoba na kuusafirisha mwili wa marehemu tarehe 2 Novemba 2009. Siku ya tarehe 5 Disemba tulimfanyia marehemu Moses Arobaini.

Malengo ya Mwaka 2010
Mwaka 2010 utakuwa mwaka muhimu sana wa Jumuiya yetu ambapo tutapitisha katiba itakayo ongoza Jumuiya yetu na pia kumchagua mwenyekiti mpya wa Jumuiya yetu. Tunategemea kufanya mkutano mkuu wa jumuiya yetu hapa Rome mwishoni mwa mwezi wa kwanza. Tutawatangazieni rasmi kupitia Blog hii siku kamili, sehemu na muda.

Kwenye Mwaka mpya 2010 pia tutalenga rasmi kwenye kudumisha zaidi mshikamano na umoja kwenye jumuiya yetu na kuifanya ijitegemee kwenye mambo mengi ya msingi. Hii yote itatokana na mwongozo mzuri wa katiba yetu ambayo itakamilika mwishonni mwa mwezi wa Kwanza.

Asanteni sana.
Mungu Ibariki Africa Mungu Ibariki Tanzania

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome
Ndg. Andrew Chole Mhella

No comments:

Post a Comment