Mkutano Mkuu wa kufunga mwaka wa Jumuiya ya
Watanzania Rome, ambao ulikuwa ukisubiriwa na Watanzania wengi tokea mjini Roma
na vitongoji vyake, ulifanyika kama ilivyopangwa saa kumi jioni jumamosi ya tarehe 24 Novemba 2012.
Mkutano ulifanyika kwenye mtaa wa Giovannni Lanza 122, mjini Roma karibia na
Kituo cha Metro cha Termini.
Mkutano huu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Roma,
uliongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Mh. Leonce Uwandameno.
Kulingana na katiba ya jumuiya ya Watanzania Roma kipengele namba 6.1, mkutano huu ufanyika
kila mwisho wa mwaka mwezi wa kumi na moja. Malengo ya mkutano kwa mwaka huu yalikuwa haya;
- Kujadili mwenendo wa jumuiya kwenye kipindi cha mwaka mzima wa 2012. Yaani
mwenendo wa michango, ushirikiano baina ya jumuiya hii ya Roma na Jumuiya
zingine za Kitanzania hapa Italy pamoja na Ubalozi wa Tanzania Italy. Wajumbe
pia walijadili mafanikio yaliyoonekana kwenye mwaka
wa 2012 na pia bila kusahau matatizo mbalimbali yaliyojitokeza na kuyatafuta
suluhisho.
- Wanajumuiya pia walijadili juu ya Utambulisho wa huduma mpya ya BIMA kwa
Watanzania waishio Diaspora. Hoja hii ilionekana kuwavutia waudhuliaji wengi
ambapo kila mmoja alichangia mawazo tofauti ambapo uongozi wa jumuiya uliwaahidi
wanajumbe kuwa utafikisha maoni yao kwa wahusika ili waweze kutoa maelezo zaidi
juu ya hii BIMA.
- Kuwasihi wanajumuiya na watanzania wote kwa ujumla, juu ya umuhimu wa
ushiriki wao kwenye kuchangia maoni kwenye mchakato mzima wa kufanikisha
ukamilishaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
Mwenyekiti, Mh. Leonce Uwandameno akisikiliza Hoja kutoka kwa mjumbe huku Katibu wake akiandika maoni ya Wanajumuiya! |
|
Katibu, ndugu Andrew Chole Mhella akielezea mwenendo wa jumuiya kwa mwaka wa 2012. |
|
Wajumbe wengi walikuwepo kwenye mkutano huu. |
|
Kwa nyuma ni Mwenyekiti Msaidizi Mh. Erasmus Pindu Luhoyo, kwa mbele kushoto ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe na Mikutano ndugu Bakari Hizza pamoja na Mjumbe Bi. Lucy M. upande wa kulia. |
|
Ndugu Mattia akionekana akisikiliza kwa makini hoja ya Mwenyekiti, kwa pembeni ni Mtoto wake Queen. |
No comments:
Post a Comment