Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania mjini Rome, Mh. Leonce Uwandameno, katikati afisa wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. Salvator Mbilinyi, na kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Ndugu Andrew Chole Mhella
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Leonce Uwandameno pamoja na Katibu wake Ndg. Andrew Chole Mhella, leo asubuhi, tarehe 23 Juni 2010, waliwasilisha rasmi barua ya utambulisho wa Jumuiya ya Watanzania Roma kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Italy. Viongozi hawa walipokelewa na afisa utawala wa ubalozi Mh. Salvator Mbilinyi. Itakumbukwa kuwa jumuiya hii ya Watanzania Roma, iliundwa rasmi mjini Rome tarehe 30 Januari 2010. Moja ya malengo mengi ya uundwaji wa Jumuiya hii ni; kuwaunganisha watanzania wanaoishi Roma na sehemu zingine za Italy, ili kushikamana na kusaidiana panapo kuwa na furaha au tatizo la aina yoyote. Jumuiya inalenga kuhamasisha wanajumuiya ili waweze kuishi kwa malengo hapa ugenini na kupeleka maendeleo nchini Tanzania. Jumuiya hii pia inalengo la kuwa chombo cha kuutangaza utamaduni na utalii wa nchi yetu hapa nchini Italia.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.
Kwa matukio mbalimbali yanayotokea hapa Rome, mnakaribishwa kwenye official blog ya Jumuiya www.watanzania-roma.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment