Pages
welcome to Tanzania
TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.
Sunday, June 27, 2010
Mkutano wa Jumuiya ya Watanzania Roma Waleta Mafanikio Mengi
Jana jioni, jumamos tarehe 26 Juni 2010, ulifanyika mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya Watanzania Roma tokea kuanzishwa kwake tarehe 30 Januari 2010. Mkutano uliudhuliwa na Watanzania wengi ambao waliweza kwa pamoja kujadili maswala mbalimbali juu ya Jumuiya kwa ujumla. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Mh. Leonce Uwandameno alifungua mkutano kwa kuwashukuru Watanzania waliofika kwenye mkutano huo muhimu kwa Jumuiya. Alitoa ufafanuzi kwa wanajumuiya wapya juu ya umuhimu wa kujiunga na Jumuiya hii. Aliwasihi wale wachache ambao walichukua mafomu ambayo bado kuyarudisha, wanaombwa wayawasilishe kwa Uongozi yaani kwa katibu au hata mwenyekiti ili waweze kutambulika kama wanajumuiya hai wa Jumuiya ya Watanzania Roma. Mwanajumuiya hai ni yule ambaye atakuwa na haki zote ambazo zimeainishwa kwenye katiba ya Jumuiya. Kikao pia kilijadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo na wanajumuiya walichangia mawazo yao ambayo yalizaa matunda kwa wingi sana na kama uongozi tukawahaidi kama tutayafanyia kazi mawazo yao. Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Jumuiya ya Watanzania Rome.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Watanzania wenzangu udumu umoja wenu. Ninaomba pia kujiunga na umoja wenu.Mtanzania mwenzenu, japokuwa nitakuwa na ugumu wa kuhudhuria vikao vyenu. Innosent Mwesigwa, Udine.
ReplyDeleteNdugu Innosent unakaribishwa sana kwenye Jumuiya yetu. Tuandikie e-mail kwa kupitia e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it au nipigie katibu kwa namba hii 3886521843 tukueleze nini cha kufanya ili uweze kuwa mmoja wa Jumuiya ya Watanzania Roma.Kumbuka umoja ni nguvu Utengano ni udhaifu!!siku njema!
ReplyDeleteAndrew Chole Mhella
Katibu