Jana, jumamosi tarehe 05-03-2016, Watanzania waishio mjini Roma waliokutana kwaajiri ya kuchagua viongozi wapya watakao ongoza jumuiya ya Watanzania Roma kwa kipindi cha miaka miwili.
Nafasi zilizokuwa zinapigiwa kura ni za Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Wajumbe wawili wa Kamati ya kuu ya utendaji.
Matokeo ni kama yafuatavyo:
1. Mwenyekiti - Ndugu Andrew Chole Mhella alishinda kwa
asilimia 90.
2. Katibu - Ndugu Sammy Kibwana alishinda kwa asilimia 55.
3. Mweka Hazina - Bi. Lilian Mashishi Luhende alishinda kwa
asilimia 80.
4. Wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji - Ndugu Kondela
Buhire na Ndugu Bedui Issa.
Kwa niaba ya viongozi wenzangu tunapenda kuwashukuru wasimamizi wa uchaguzi, ndugu Raymond na ndugu Yohana Shija Masalu kwa kusimamia vizuri zoezi zima la uchaguzi.
Tunapenda kuwafahamisha Watanzania wote wa Roma kuwa Katiba na mafomu ya kujiunga na Jumuiya yapo tayari kwa wale ambao bado hawajapata nafasi ya kuyachukua watuinbox tuweze kuwafahamisha namna ya kuyapata mafomu na pamoja na katiba.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.
Andrew Chole Mhella
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma.
No comments:
Post a Comment