Tunapenda kuwafahamisha wana diaspora kuwa, Hospitali ya Agakhan ina mahitaji ya haraka sana ya wataalamu wa Afya kuziba nafasi mbalimbali za kitabibu zilizo wazi katika hospitali hiyo. Hospitali hiyo imetoa kipaumbele kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kujaza nafasi hizo, baada ya kukosekana kwa wataalam wa kutoka nchini Tanzania.
Tafadhali wafahamisheni watanzania walioko katika eneo lenu waombe nafasi hizo kwa wingi ili kujaza nafasi husika kama zilivyoainishwa kwenye Tangazo la Ajira lililoambatishwa. Maombi hayo yatumwe kabla ya tarehe 6 Februari 2016, kupitia barua pepe ifuatayo: mary.mlay@akhst.org, nakala kwa diaspora@nie.go.tz, na info@embassyoftanzaniarome.info.
No comments:
Post a Comment