UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA UNAPENDA KUWAFAHAMISHENI KUWA, MWILI WA MAREHEMU THOMAS RYNOS PETER A.K.A KIGADI, UTAAGWA KESHO ASUBUHI, TAREHE 07/12/2015 KWENYE MORTUARY YA POLICLINICO UMBERTO I KUANZIA SAA NNE MPAKA SAA TANO NA NUSU ASUBUHI. BAADA YA HAPO TUTAKUTANA KWENYE UKUMBI ULIOPO MTAA WA VIA MAGENTA 53 KUANZIA SAA SABA MPAKA SAA KUMI KWAAJIRI YA SADAKA NA KUOMBOLEZA. MWILI WA MAREHEMU UTAONDOKA SIKU YA JUMANNE TAREHE 08/12/2015 NA TURKISH AIR KWENDA TANZANIA KWAAJIRI YA MAZISHI. KWA NIABA YA JUMUIYA ZOTE ZA WATANZANIA ITALY TUNAPENDA KUWASHUKURU WALE WOTE MLIOKUWA MSTALI WA MBELE KWENYE SAFARI NZIMA YA MAANDALIZI YA KUMSAFIRISHA NDUGU YETU KIGADI.
TUNAOMBA TU WALE AMBAO BADO HAWAJAKAMILISHA MICHANGO YAO WAJE NAYO KESHO MOJA KWA MOJA KWENYE ENEO LA TUKIO.
ASANTENI SANA.
Katibu,
Andrew Chole Mhella
No comments:
Post a Comment