Maofisa wa Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam na
Zanzibar wameanza zoezi la kupokea maombi ya pasipoti kutoka kwa Watanzania
waliopo Italy. Maofisa hao wanategemewa kuelekea Turkey na Greece,kwa ajili hiyo
hiyo. Haya ni matunda ya Kamati ya Diaspora ilyokutana na Mh Balozi James Alex
Msekela, mwezi juni mwaka huu. Kamati ilikutana na balozi na maofisa wa juu wa
kibalozi kwa ajili ya kutambulisha kamati na uongozi wake,na pia kuwakilisha
kero na matatizo ya watanzania wanaoishi Italy kwa jumla. Mkutano huo uliisha
kwa mafanikio makubwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya uchapa kazi wa kweli wa mh
Balozi, kwani katika mapumziko yake nchini Tanzania mwezi August alitumia muda
wake kukutana na Kamishna wa Uhamiaji Tanzania kujadili suala la matatizo ya
Pasipoti kwa watanzania wa Maeneo ya uwakilishi wake.
Source: JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA (JUWATAI) http://watanzaniaitalia.blogspot.it/2014/11/zoezi-la-maombi-ya-pasipoti-linaendelea.html?spref=fb
Source: JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA (JUWATAI) http://watanzaniaitalia.blogspot.it/2014/11/zoezi-la-maombi-ya-pasipoti-linaendelea.html?spref=fb
No comments:
Post a Comment