Siku ya jana, tarehe 18 Novemba 2014 kwa Watanzania Italy, imeingia kwenye historia baada ya Watanzania kupata fursa ya kukutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mohamed Gharib Bilal . Mkutano ulidhuliwa na msafara mzito aliokuja nao Makamu wa Rais wakiwemo mawaziri, balozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. James Alex Msekela, maofisa wa ubalozi, viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Tanzania nchini Italy pamoja na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italy.
|
Gari lililombeba Makamu wa Rais, Mheshimiwa Mohamed Gharib Bilal. Hapa likiwa limepakiwa katika Hotel ya EDEN. Hotel aliyofikia Mh. Makamu wa Rais. |
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora Italy, Mh. Maulid Kagutta akitoa risala kwa niaba ya Wanadiaspora Italia. |
|
Meza Kuu Wakati wa Mkutano kama inavyoonekana. |
|
Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. James Alex Msekela akipata picha pamoja na Makamu wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mama Bilal. |
|
Watanzania wakisalimiana na Makamu wa Rais. |
|
Picha ya pamoja na Makamu wa Rais.
Kwa yeyote ambaye anapicha zaidi za tukio ili tafadhali anitumie kwenye e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it ili tuweze kuzitundika! Thanx!!
|
No comments:
Post a Comment