Watanzania waishio Mjini Roma, Jana jioni tarehe 12 aprili 2014 walikutana kwenye ukumbi wa Wahindi uliopo Via Principe Amedeo mjini Roma, kujadili maswala mbalimbali yanayowagusa Watanzania kwa ujumla. Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma, ambao ndio ulichukua jukumu la kuongoza mkutano huu, ulikuwa na lengo kuu la kuwakumbusha Watanzania waishio mjini Roma umuhimu wa Kujiunga na Jumuiya. Mwenyekiti na Katibu walisisitiza sana kwenye kuwaelimisha wale ambao hawajafunguka, juu ya umuhimu wa kujiunga na Jumuiya. Katika kutoa motisha, Katibu, ndugu Andrew Chole Mhella alieleza kuwa, Jumuiya ni chombo muhimu sana kwa sisi Watanzania tuishio ughaibuni, aliendelea kusema kuwa ni chombo cha kuwakutanisha Watanzania ili waweze kufahamiana, kusaidiana, na kutatua matatizo mbalimbali ya yanayowapata. Kwa hiyo basi kwa kujiunga na jumuiya aliendelea Katibu, utatambulika rasmi kuwa ni mmoja wa wanajumuiya na utakuwa na haki ya kusaidiwa kama mwanajumuiya. Haki ambayo watanzania wengi mjini Roma wanaikosa. Katibu alendelea kusema kuwa hapa mjini Roma, Watanzania wengi wamekuwa wakiutafuta na wamekuwa wakiona umuhimu wa Jumuiya pale tu wanapokuwa na matatizo, kama vile ugonjwa , kifo, shida ya passport na na matatizo mbalimbali ya kisheria.
Kabla ya kufunga kikao, Katibu aliwaomba wale wote wanataka kujiunga na jumuiya wamwandikie e-mail: watanzaniaroma@yahoo.it au kumpigia Katibu simu kwa namba hii 3391597134 ili aweze kuwapa copy ya Katiba pamoja na fomu la kujiunga! Kikao kijacho kitakuwepo mwanzoni mwa mwezi tano. tarehe kamili mtatangaziwa.
No comments:
Post a Comment