Napenda Kuchukua nafasi hii kuwashukuru wajumbe wote walionichagua kuwa katibu wa Kwanza wa Kamati ya Diaspora nchini Italy, siku ya jumamosi, tarehe 8 February 2014 Mjini Napoli! Hatua ya kunichagua imeonyesha ni jinsi gani mmependezeshwa na utendaji wangu wa kazi! Nami nawahikikishieni kuwa kwa kushirikiana na Mh. Mwenyekiti na wajumbe wote, nitajitaidi kadri ya uwezo wangu kuwawakilisha vizuri na pamoja na viongozi wengine, tutayafanyia kazi yale yote mliotuomba tuyafanyie kazi! Mwenyezi Mungu aibariki Tanzania na Wanadiaspora wake!.
Hawa hapa ndio Viongozi wa Kamati ya Kwanza ya Diaspora Italy.
- Hon. Nsangu Maulidi Kagutta
- Hon. Ricky Bondo ( Mwenyekiti Msaidizi )
- Mr. Andrew Chole Mhella ( Secretary )
- Lilian Luhende ( Mweka Hazina )
Na. Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Pamoja na Katibu wa Kamati ya Diaspora Italy.
|
Wanakamati Wote kwa Pamoja |
|
Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma wakipata Lunch |
|
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italy pamoja na Mweka Hazina wa Kamati ya Diaspora Italy Bi. Lilian Luhende |
|
Kushoto ni mjumbe wa Kamati ya Diaspora Italy, ndugu Kondela Buhure pamoja na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome pamoja ambaye pia ni Katobu wa Kamati ya Diaspora Italy, ndugu Andrew Chole Mhella |
|
Pichani: Katibu mpya wa Kamati ya Diaspora Italy ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome Ndugu Andrew Chole Mhella akizawadiwa cheti cha shukrani kwenye utendaji kazi na mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy. |
|
Ujumbe tokea Rome |
No comments:
Post a Comment