Jumuiya za
Watanzania Italy, kwa pamoja walifanya mkutano mkuu wa kihistoria siku ya
jumamosi tarehe 8/2/2014.
Mkutano
huo uliofanyika mjini Napoli,ulikuwa na madhumuni matatu makubwa.
kwanza
kuimarisha mshikamano baina ya Jumuiya za Watanzania nchini Italy, na pili
kuzungumzia kero na matatizo ya Watanzania wanaoishi Italy.Wajumbe walichangia
yote yaliyokusanywa katika mikutano na vikao vya awali.
Yote
yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi na kufikishwa kunakostahili kwa ufumbuzi wa
kudumu.
Jambo
kubwa la tatu, Wajumbe waliunda kamati ya pamoja ya diaspora yenye wajumbe
kutoka NAPOLI,ROMA,MODENA,GENOVA NA PADOVA. Na kuweka majukumu. Wajumbe pia
walimchagua:
Ndugu Kagutta N.Maulidi (Mwenyekiti)
Ndugu Ricky JG.Bondo ( kaimu m/kiti)
Ndugu Andrew Chole Mhela (katibu)
Ndugu Mwinyimwaka Sarai (kaimu/katibu),
Ndugu LIlian Luhende (hazina)
Ndugu Abdulrahaman A.Alli (mjumbe)
Ndugu Erasmus Luhoyo (Mjumbe)
Ndugu Livinus Mwereke (Mjumbe)
Ndugu Awadhi Sulaiman (Mjumbe)
Ndugu Judith Joseph (Mjumbe)
Ndugu Zacharia
Madjid Mhessa (Mjumbe)
Wajumbe
wa mkutano wamependekeza kuwa baada ya kipindi cha miaka miwili utafanyika
mkutano wa kutathmini utendaji wa kamati kwa ujumla.
Mwisho
mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy mh Abdulrahaman A.Alli aliwapongeza
baadhi ya viongozi na wajumbe kwa kuwatunukia shahada za uongozi bora na
uhadilifu.
Source: Jumuiya ya Watanzania Italy
(www.watanzaniaitalia.blogspot.it)
Pichani Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh Abdulrahaman A.Alli(aliyeshika cheti) akimtunukia cheti cha uadilifu na uongozi bora Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Andrew Chole Mhela. |
Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora Mh. Kagutta N.Maulidi akionyesha cheti alichotunukiwa na mh Mwenyekiti kwa uadilifu na uongozi bora wa jumuiya ya Watanzania Italy . |
Wajumbe wakifuatilia mkutano kwa makini |
viongozi katika picha ya pamoja |
hii ndio kamati ya Diaspora |
Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati. |
Kaimu Mwenyekiti wa Diaspora Mh Ricky JG.Bondo akifafanua jambo kwa mjumbe ndugu Mohamed Mnondwa, baada ya kikao. |
No comments:
Post a Comment