Watanzania nchini Italy leo asubuhi , tarehe 20 Januari 2014,
walijumuika kwa pamoja kwenye Policlinico Tor Vergata iliyopo mjini
Rome kwaajiri kuuga mwili wa marehemu Ally Kijuu Juma, aliyefariki mjini
Roma tarehe 31 Dicemba 2013. Mwili wa marehemu unategemewa
kusafirishwa kesho na SAUDI AIRLINES kwenda nchini Tanzania kwa mazishi!
Kwa mara nyingine tena Watanzania nchini Italy wameonyesha mshikamano
wa hali ya juu kwenye kufanikisha hii shughuli ya usafirishaji wa mwili
wa marehemu! Itakumbukwa kuwa Kwenye kipindi cha mwezi mmoja na nusu
watanzania nchini Italy wamepatwa na misiba minne na kwa upendo na
mshikamano wa hali ya juu, wamefanikiwa kuwasafirisha marehemu wote
kwenda kupumzika kwa amani nchini Tanzania.
Uongozi wa jumuiya ya watanzania Rome pamoja na uongozi wa jumuiya ya Watanzania Italy, unapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa Watanzania wote wamjuaye na wasiojua marehemu kwenye kufanikisha zoezi ili.
Mwenyezi Mungu azilaze roho
za hawa marehemu mahali pema peponi. Amen.
No comments:
Post a Comment