MKUTANO WA WATANZANIA ROMA
Jumuiya ya Watanzania Roma jumamosi ijayo tarehe 25 January 2014 imeandaa mkutano kwaajiri ya Watanzania wote waishio Roma. Mkutano huu ambao unategemewa utaudhuliwa na Wanajumuiya na wale ambao si wanajumuiya,utafanyika kwenye Restaurant ya Kihindi iliyopo kwenye Mtaa wa Via Principe Amedeo saa kumi jioni. Agenda ya Mkutano huu kwanza kabisa ni kuweza kufahamiana, maana tunaamini kuwa Mjini Roma kuna Watanzania wengi sana ila shida ni kwam...ba baadhi ya Watanzania wamekosa chombo cha kuwaunganisha na Watanzania wengine waishio Roma na sehemu nyingine nchini Italy. Agenda ya pili ambayo ni muhimu zaidi ni kuweza kujadilii kwa pamoja matatizo na kero mbalimbali ambayo Watanzania tunapata hapa nchini Italy na kujaribu kwa pamoja kutafuta njia ya kutatua haya matatizo. Tunaomba tufike kwa wingi maana sisi kama viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma tutachukua mawazo yenu na kwenda kudiscuss na viongozi wa Jumuiya zingine hapa hapa Italy na kuweza kupata njia ya kutatua haya matatizo. Mnaombwa mje kwa wingi maana mkutano huu unalengo la kutatua matatizo yetu sisi sote kwa ujumla!
Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome

No comments:
Post a Comment