KWA NIABA YA UONGOZI WA JUMUIYA YA
WATANZANIA ITALIA NA JUMUIYA YA WATANZANIA ROME, NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII
KUWASHUKURA WOTE WALIOCHANGIA KWA NJIA MOJA AU NYINGINE KATIKA KUFANIKISHA MSIBA
HUU. LEO TUMEKUSANYIKA MJINI NAPOLI KUUAGA MWIL...I WA MAREHEMU
MAULIDI HAMID ABDALLAH (KIDISHI) ALIYEFARIKI HOSPITALINI BAADA YA KUUGUA KWA
MUDA MFUPI. RATIBA YA NDEGE ITAKAYOCHUKUA MWILI WA MAREHEMU TUTAWATANGAZIA.
NAPENDA KUWAKUMBUSHA KUWA SIKU YA JUMATATU MJINI ROME WATANZANIA WATAJUMUIKA
TENA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU JUMA KIJUU NAE ALIFARIKI ROME. TUNAUNGANA NA
WAZAZI, NDUGU NA JAMAA WA MAREHEMU WETU KATIKA KUOMBOLEZA MISIBA HII YA NDUGU
ZETU WALIOONDOKA KUJA UGHAIBUNI KATIKA KUTAFUTA MAISHA. KWA WALE WANAOISHI
NAPOLI KAMA KAWAIDA BASI LITAONDOKA NAPOLI MJINI SAA KUMI NA MBILI ASUBUHI NA
KUPITA VITUO VYA KAWAIDA NA KITUO CHA MWISHO LITAONDOKA SAA MOJA NA NUSU. MUNGU
AWALAZE MAHALA PEMA AMEEN!!!!!!!
Kagutta N.M
Kagutta N.M
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Italy
Source: Jumuiya ya Watanzania Italy - (www.watanzaniaitalia.blogspot.it)
No comments:
Post a Comment