Uongozi wa Jumuiya ya
Watanzania Roma Jana tarehe 25 Januari 2014, uliongoza mkutano wa
Watanzania waishio mjini Rome.Mkutano huu ulikuwa na lengo la
kuwashukuru wale wote walioshiriki na kuchangia kwa namna moja au
nyingine kwenye kufanikisha usafirishaji wa miili ya marehemu (3) kwenda
nchini Tanzania kwa mazishi. Mkutano pia ulikuwa na lengo kuwawezesha Watanzania mjini Rome kufahamiana na zaidi
kubadilishana mawazo juu ya maswala mbalimbali yanayowakabiri Watanzania
nchini Italy, zikiwemo kero na matatizo mbalimbali. Uongozi wa
Jumuiya Unapenda kuwashukuru wale wote waliuodhulia mkutano huu na
kuwahakikishia kuwa yale yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi kikamilifu.
Safari bado ni ndefu ila penye nia pana njia!
Safari bado ni ndefu ila penye nia pana njia!
No comments:
Post a Comment