LEO TAREHE 30 JANUARI 2014, JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA IMETIMIZA MIAKA MINNE TANGU KUANZISHWA KWAKE HAPO TAREHE 30 JUNUARI 2010! KWENYE HII MIAKA MINNE, TUMEWEZA KUPATA MAFANIKIO MENGI SANA KAMA VILE: KUWA KIUNGO CHA WATANZANIA WAISHIO MJINI ROMA NA SEHEMU ZINGINE ZA HAPA ITALY, TUMEWEZA KUIMARISHA USHIRIKIANO WETU NA JUMUIYA MBALIMBALI ZA WATANZANIA HAPA NCHINI ITALY NA NJE YA ITALY, TUMEWEZA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA MBALIMBALI ZA WATANZANIA HAPA ITALY KWENYE SHIDA NA RAHA, TUMEWEZA KUUTANGAZA UTAMADUNI WA TANZANIA HAPA NCHINI ITALY PAMOJA NA MENGINEYO. HIVI SASA KWA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY TUPO KWENYE HATUA NZURI YA KULETA MAENDELEO ZAIDI SI KWA WATANZANIA WAISHIO NCHINI ITALY BALI HATA KWA WATANZANIA WALIOPO NCHINI TANZANIA. MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE. PICHA ZOTE ZIMIETOKA KWENYE MAKTABAYA JUMUIYA.
KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA, NDUGU ANDREW MHELLA AKIWAKARIBISHA KWENYE MEZA KUU NDUGU ANDREW KYABASHASA NA MH. MBILINYI TAYARI KUANZA MKUTANO.
PICHA HII ILIPIGWA WAKATI WA
KUPITIA KATIBA. KUSHOTO NI NDUGU ANDREW
CHOLE MHELLA AMBAYE ALICHAGULIWA KUWA KATIBU, KATIKATI NI NDUGU ANDREW
KYABASHASA AMBAYE ALIKUWA MUONGOZAJI WA MKUTANO NA KULIA NI MH. MBILINYI
AMBAYE ALIKUWA OBSERVOR TOKA UBALOZI WA TANZANIA ITALY.
WAKATI WA CHAKULA.
No comments:
Post a Comment