MKUTANO WA MSIBA MJINI NAPOLI
Watanzania leo walikutana chini ya uongozi wa
Jumuiya ya Watanzania Italia, kupata taarifa rasmi ya kifo cha marehemu ABDULLI
ABUU ( HATIBU CLEAN HEART) na kupanga mikakati ya mazishi. Uongozi wa jumuiya ya
Watanzania Italia uliongozwa na katibu mkuu wa Jumuiya ndugu Kagutta N.Maulidi,
akiwa pamoja na Katibu wa Napoli ndugu Livinus Mwereke na katibu mipango wa
jumuiya ndugu Mohamed Abdulwahab, viongozi walito muhtasari wa kifo cha marehemu
na wajihi wake,pamoja na hayo pia walitoa taarifa iliyotoka kwa wazazi wa
marehemu kupitia kwa mwenyekiti wa jumuiya ambae kwa wakati huu yuko Tanzania
kikazi. ilielezwa pia kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia ndugu
Abdulrahamani A.Alli atakuwa na kikao na wazazi wa marehemu kesho jumapili ili
kuwapa taarifa na taratibu zinazofanywa na Watanzania chini ya Jumuiya za
Watanzania Italia.
Marehemu alifariki mjini Rome siku ya tarehe 8/12/2013. Tayari taarifa ya msiba imeshatolewa kwa Balozi wa Tanzania Italy uliopo Rome, Taarifa hizo zilifikishwa jana na Katibu wa jumuiya ya Watanzania Rome ndugu Endrew Mhela, baada ya kutambua mwili wa marehemu, hospitali na sehemu ulipo. Vilevile taarifa zilizoletwa na ndugu Mhela kuwa tayari amekwisha wasiliana na wakala wa usafiri kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu Hatibu cleanheart nyumbani Tanzania kwa mazishi.
Tayari michango imesha anza kukusanywa,ndugu Livinus Mwereke aliwahimiza Watanzania wote kujitolea zaidi ili kuharakisha taratibu za kusafirisha mwili ili kwenda na muda kabla haujapinduka mwaka. Taarifa zilisema pia kuwa Jumuiya ya Watanzania Rome watakuwa na mkutano na watanzania siku ya jumanne,vilevile Modena na Genova. Kwa yeyote mwenye nia ya kuchangia kwa walioko mbali yaani nje ya Italy wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome ndugu Mhella ambae ndie anaesimamia mpango mzima.
Mungu amlaze mahala pema peponi Ameen!!
mawasiliano: 0039 339 1597134
Source:Jumuiya ya Watanzania Italy- www.watanzaniaitaly@blogspot.it

WATANZANIA WAKISIMAMA KIMYA KWA DAKIKA ISHARA YA HESHIMA NA KUMUOMBEA MAREHEMU KABLA YA KUANZA KWA MKUTANO. |
No comments:
Post a Comment