Mwili wa Marehemu Tofiki Saidi Mpira ambao ulisafirishwa Tokea Rome, Italia, kwenda Dar-es-Salaam, Tanzania, uliwasili salama jumamosi 13 Julai na kupokelewa na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Marehemu alizikwa siku ya jumatatu ya tarehe 15 Julai.
Kwa niaba ya ndugu wa Marehemu, Mh.Abdulrahamani A.Alli (Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italy), anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa:
1. Ubalozi wa Tanzania Italy, kwa ushirikiano mkubwa waliuonyesha.
2. Viongozi wa jumuiya za Watanzania nchini Italy (Jumuiya ya watanzania Italia pamoja na Jumuiya ya Watanzania Roma).
Pia shukrani za dhati ziende kwa Watanzania wote waliojitokeza kutoa msaada wa aina yoyote ile ambao umesaidia kuwezesha usafirishaji wa mwili wa marehemu kwenda kupumzishwa kwa amani nchiniTanzania.
Shukrani kubwa pia ziende pia kwa viongozi na wanachama wote wa Club ya Wazee wa Magomeni kwa kushiriki kikamilifu katika matayarisho yote ya mapokezi ya mwili pamoja na maziko bila kuwasahau
ndugu Jabir Suleiman Mwalimu, ndugu Daniel Darra na ndugu Abasi.s.cooker.shukran kwa m/kiti na katibu ndugu Madohora wa serikali ya mtaa wa DOSI kata ya magomeni.
No comments:
Post a Comment