Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Friday, May 18, 2012

WATANZANIA ROMA WAUAGA MWILI WA MAREHEMU FR. JAMES A. MBWANA

Leo tarehe 18 Mei 2012, Watanzania kutoka kila kona ya Roma, wakiongozwa na balozi wa Tanzania nchini Italia, Mheshimiwa James Msekela, pamoja na marafiki mbalimbali wa marehemu James A. Mbwana, walikusanyika kwenye misa takatifu ya kuuaga mwili wa  marehemu aliyefariki gafla jumatano tarehe 16 mei 2012 maeneo ya Termini mjini Roma akiwa njiani kuelekea Chuoni kama ilivyokuwa kawaida yake. Misa hii imefanyika katika parokia ya Mtakatifu Francisco jimboni Palestrina mjini Roma ambako marehemu alikuwa akitumikia na kuishi sambamba na kufuatilia masomo yake katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kilichopo mjini Roma.  Misa iliongozwa na Mhasham Askofu Dominic, Askofu wa Jimbo la Palestrina.
Habari zaidi juu ya lini mwili wa marehemu utaondoka tutawapatieni kadri tutakapo zipata. Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Roma tunawapa pole sana ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa ambao unatukumbusha kuwa sisi binadamu hapa duniani ni wapita njia tu. Siku yoyote mwenyezi Mungu anaweza kutuchukua. Kwa hiyo hatuna budi kujiandaa kwa kusali na kutenda mema mbele ya mwenyezi Mungu.
 Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake liidimiwe milele amina!

                Jeneza la Marehemu Fr. James Mbwana likiwa kanisani wakati wa misa.

        Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela pamoja na Mwenyekiti wa 
             Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Leonce Uwandameno wakati wa ibada takatifu.

                                                                   Ibada ikiendelea.
Mwili wa Marehemu James Mbwana Ukitolewa kanisani na mapadri wakitanzania.
Baada ya misa kuisha.

                     Mh. Balozi akilonga na Paroko wa parokia aliyokuwa anakaa marehemu.

Picha zote na Fr. Flavian Kassala

 

No comments:

Post a Comment