
Ile sherehe ya Muungano wa Tanzania na Utamaduni wake, ambayo mwaka jana ili fana sana mjini Roma, mwaka huu itakuwepo tena. Maandalizi kabambe yameanza na Watanzania wote kwa pamoja mnaombwa kushiriki kwa namna moja au nyingine. Sherehe imepangwa kufanyika tarehe 28 April kwenye Ukumbi uitwao KALISPERA CLUB 69, uliopo Via Angelo Emo 69/A-B mjini Roma. Safari hii tutajirusha mpaka lyamba. Sherehe itaanza saa kumi na moja jioni mpaka saa kumi na nusu asubuhi. Muda huu umepangwa kutokana na maombi ya Watanzania wengi. Safari hii kutakuwa na zawadi nono kwenye bahati na sibu ambayo itatangazwa pale itakapo kuwa tayari, muziki safi wa kitanzania, vyakula na maonyesho ya mavazi ya Kitanzania.Ili kuweza kufanikisha sherehe hii na ili muweze kupata maelekezo ya namna ya kushiriki, tafadhali wasilianeni na Mwenyekiti Leonce Uwandameno kwa kupita ubalozini, Katibu Andrew Chole Mhella 3479094800 au Mweka Hazina Ndugu Awadhi 3458352262 au kwa e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.it.
Asanteni na mungu Ibariki Tanzania.
(Please click the advert to enlarge it. Tafadhali bonyeza Tangazo kuongeza ukubwa.)
No comments:
Post a Comment