Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome, ndugu Andrew Chole Mhella leo asubuhi(14/07) amekutana na mdau mkubwa ajulikanaye na wengi kupitia mtandao wa Issa Michuzi (www.issamichuzi.blogspot.com)ndugu Baraka Chibiriti aishie Mjini Siena. Bwana Chibiriti ambaye alikuwa jiani kuelekea Tanzania kwa shughuli binafsi alimuambia ndugu katibu kuwa anafurahishwa sana na jinsi blog ya Jumuiya ya Watanzania Rome inavyoendeshwa na kwa ujumla mipango mizima ya Jumuiya ya Watanzania Roma. Bwana Baraka Chibiriti amemdokozea katibu kuwa muda si mrefu mambo yakienda kama yalivyopangwa atatuletea mgeni mmoja muhimu sana Tanzania kuja kututembelea wanajumuiya. Jina kwa sasa limewekwa kapuni mpaka pale mipango itakapo kamilika.
Mnaweza kumtembelea blog ya ndugu Chibiriti hapa:
http://makalala-chibiriti.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment