
Jumuiya ya Watanzania Rome inaungana pamoja na Watanzania popote pale walipo duniani kushurekea miaka 49 ya uhuru wa Tanzania bara. Itakumbukwa kuwa Tanzania Bara au kwa kipindi kile Tanganyika, ilipata uhuru kutoka kwenye utawala wa Kiingereza tarehe 9 Disemba 1961 chini ya usimamizi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Sisi Watanzania tuna kila haki zote za kujivunia uhuru wetu si tu kwa namna tulivyoupata bali kwa namna ambayo tumeutunza na kuuheshimu mpaka siku hii ya kusherekea miaka 49. Watanzania tunatumiwa kama mfano wa kuigwa na nchini nyingi za Africa kutokana na jinsi tunavyoheshimu na kutunza yale mazuri tuliyoachiwa na wazee wetu wa Taifa. Hii yote ni kwa sababu mpaka hii leo kunanchi nyingi tu Africa hazipatani japo ya kuwa na uhuru. Watanzania pia hatuna lazima tujivunie pia matunda ambayo baba wa Taifa alitupandia kabla,wakati, na baada ya kupata uhuru.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa.
No comments:
Post a Comment