Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Thursday, August 12, 2010

Mwili wa Marehemu Hamisi Abdalla George Wazikwa Dar (12/08/2010)

Mwili wa marehemu Hamisi Abdalla George (Mmakua) aliyefariki mjini Rome, Italy tarehe 18/07/2010 uliwasili juzi tarehe 11/08/2010 kwenye uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar-es-Salaam na shirika la ndege la Emirates na kuzikwa jana jioni tarehe 12/08/2010 kwenye makaburi ya Mbagala Maji Matitu. Mwili wa marehemu ulipokelewa na mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Rome ndugu Andrew Kyabashasa, ambaye ni mwanajumuiya hai wa Jumuiya ya Watanzania Rome, pamoja na ndugu wa marehemu. Ndugu wa marehemu wametoa shukrani zao za dhati kwa kamati nzima ya usafirishaji wa mwili wa marehemu ikiongozwa na Jumuiya ya Watanzania Rome chini ya usimamizi wa Mweyekiti msaidizi Mh. Erasmus Luhoyo pamoja na ndugu Andrew Chole Mhella wakishirikiana na jumuiya ya watanzania Modena chini ya uongozi wa ndugu Mwinyimwaka Hatibu, Genova chini ya ndugu Ricky Bondo, Napoli chini ya Mwandai pamoja na kwa maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy na kwa ujumla wale wote waliojitoa kwenye kufanikisha shughuli nzima ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kupumzika kwa amani nchini Tanzania.Nae Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Rome ndugu Andrew Kyabashasa kwa niaba ya Jumuiya alitoa pole kwa wafiwa na kuwashukuru kwa ushirikiano waliouonyesha kwenye kufanikisha kumsafirisha marehemu. Mwenyezi mungu amlaze marehemu mahali pema peponi amina.
Mwili wa Marehemu ukiwa airport tayari kukabidhiwa kwa mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Roma, ndugu Andrew Kyabashasa na ndugu wa marehemu.
Mwili wa Marehemu ulipowasili Nyumbani kwa marehemu Mbagala tayari kwa mazishi.
Marehemu akiombewa Dua.
Hii ni nyumba ya marehemu aliyoijenga mbagala lakini hakupata bahati kuiona.Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Rome akiwakilisha salama za Pole kutoka mjini Rome.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Roma, ndugu Andrew Kyabashasa akishiriki kwenye kufunika kaburi la Marehemu Hamisi Abdalla George.

1 comment:

  1. Apumzike kwa amani marehemu Hamisi Abdallah George. Hatimaye amepumzika kwake! Pongezi za dhati kwa mshikamano na umoja ulifanikisha kumrudisha nyumbani marehemu Hamisi. Leonce uwandameno.

    ReplyDelete