
Marehemu Mmakuwa Wakati wa Uhai Wake.
Kamati kuu ya maandalizi ya kusafirisha mwili wa Marehemu Hamisi Abdallah George(Mmakua) aliyefariki tarehe 18 julai 2010, saa tatu na dakika ishirini na tano usiku (21:25), ikiongozwa na Jumuiya ya Watanzania Roma kwa ushirikiano na Jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Italy na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy, inapenda kuwafahamisha Watanzania wote mliopo nchini Italy kuwa mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumamosi tarehe 31 Julai 2010 saa sita mchana(12:00) kabla ya kwenda kupumzika kwa amani nchini Tanzania. Mwili utaagwa kwenye Istituto Lazzaro Spallanzati, iliyopo nyuma ya Ospitali ya San Camillo, kwenye mtaa wa Via Folchi 6/a, mjini Roma. Watanzania wote mnaombwa mfike ili tumuombee na tumuage marehemu. Kwa wanaotokea Termini mnaweza kuchukua BUS H mpaka kwenye kituo cha San Camillo halafu mnaweza kuchukua bus 774 au 228 na kushuka kituo cha 3.
No comments:
Post a Comment