
Jana usiku timu ya AC Roma, ilitoka kidedea kwenye DERBY la mji mkuu, wenyewe waliita DERBI DI CAPITALE, baada ya kuifunga Lazio kwa mabao 2-1. Mechi ilikuwa nzuri sana na wenyeji ambao walikuwa lazio walifunga bao la kuongoza katikati kipindi cha kwanza. Goli lililofungwa na mshambuliaji Rocchi. Muda si mrefu Lazio wakipewa Penati ambayo ilipanguliwa na kipa wa Roma. Kipindi cha pili Roma walianza vizuri na kusawazisha na Vucinic kwa njia ya penati na muda si mrefu kupachika bao la pili lililofungwa na tena na Vucinic. Honi za magari zilisikika kila kona ya mji baada ya mpira na sehemu mbalimbali ilikuwa na kelele za ushangiliaji wa ushindi huu ambao umeiwezesha Roma kuendelea kuongoza ligi ikiwa na point moja zidi ya Inter na point saba zaidi ya AC Milan.Mechi zimebaki nne, sasa tuone itakuwaje!
No comments:
Post a Comment