
Leo Jioni alhamis 18 March, kwenye kanisa Kuu la Mtakatifu Petro(Saint Peters)Mwadhama Kardinali Tarcisio Bertone ambaye ni Katibu wa Vatican, kwa niaba ya Baba Mtakatifu amewasimika Uaskofu mkuu watumishi watatu wa Kanisa Takatifu Katoriki. Kwanza kabisa kwa Mtanzania Monsignor Novatus Rugambwa ambaye ni Askofu Mteule wa Tagaria ambaye pia ni Nunzio Mteule (Mwakilishi wa Vatican) nchini Angola na Sao Tome' na Principe. Wapili ni Monsignor Pietro Piopo askofu Mteule wa Torcello na mteule Nunzio wa Cameroun na Guinea na Watatu ni Monsignor Eugene Martin Nugent Askofu mteule wa Domnach Sechnaill na ambaye ameteuliwa kuwa Nunzio wa Madagascar, Mauritus na Shelisheli. Ibada hii takatifu iliudhuriwa pia na Askofu wa Bukoba Monsignor Nestorius Timanywa. Sisi Kama Jumuiya ya Watanzania Rome tunampa hongera na kumtakia mafanikio mema Baba Askofu mteule na Nunzio Apostolico Novatus Rugambwa kwenye Wadhifa huu mpya.
Hongerasana mhashamu Novatus Rugambwa. Safari na utume mwema huko Angola. New York City
ReplyDelete