
Rome:28/Feb.Leo jioni viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome (Mwenyekiti Leonce Uwandameno, Mwenyekiti Msaidizi Erasmus Luhoyo na Katibu ndugu Andrew Chole Mhella) walipata nafasi ya kukutana na viongozi wa Umoja wa Wanafunzi Watanzania Wakatoliki Roma. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kutambulishana, kufahamiana na zaidi kuangalia uwezekano wa kushirikiana pale panapo kuwa na sherehe za kitaifa, ugeni muhimu tokea Tanzania, na zaidi namna ya kushirikiana pale panapo kuwa na mgonjwa au msiba wa Mtanzania. Pande zote mbili zilifurahishwa na matokeo ya mkutano na kuhaidi kushirikiana kwenye maswala yaliyojadiliwa. Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment