
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma unapenda kuwatangazia Watanzania wote muishio Roma na Italia kwa ujumla kuwa Katiba na fomu za kujiunga na jumuiya zipo tayari na zinapatikana kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ambaye mnaweza kwenda kuchukua kwake ubalozini au mnaweza kumwandikia Katibu kupitia e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.com, ambaye atawatumieni haraka iwezekanavyo. Mtakapo rudisha fomu mnatakiwa kuambatanisha picha ya passport na ada ya kujiunga ambayo ni euro 20. Asanteni - Katibu
No comments:
Post a Comment