

nyuma yao ni Bwana Fedha Awadhi!
Rome: Jana tarehe 30 Januari, Mjini Rome, Italy, kulikuwa na mkutano mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Roma. Mkutano huu ulikuwa na agenda mbili, kwanza: Kupitisha Katiba ya Jumuiya ya Watanzania Roma; pili, kuchagua Viongozi. Mkutano uliudhuliwa na Mh. Salvator Mbilinyi, ofisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy ambaye alimuwakilisha Mh. Ali Abeid Aman Karume, balozi wa Tanzania nchini Italia. Waliochaguliwa kuwa Viongozi ni ndugu Leonce Uwandameno kama mwenyekiti wa Jumuiya, ndugu Erasmus Luhoyo Pindu, kama mwenyekiti Msaidizi, Diana Olotu kama Katibu msaidizi. Katibu na Mweka hazina wamebaki wale wale yaani Katibu Ndugu Andrew Chole Mhella na Mweka Hazina ndugu Awadhi.Wajumbe wakiochaguliwa ni Wawili Ndugu Boniface Mhella na Bi. Khadija Kirro.Mwenyekiti baada ya kuchaguliwa aliwashukuru wanajumuiya kwa kumpatia wadhifa huo na kuhaidi kushirikiana na wanajumuiya wote kudumisha na kuimalisha Jumuiya.
No comments:
Post a Comment