Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Tawi la Roma unapenda kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliofika kumuaga Marehemu Moses Kiumbi jana tarehe 31 oktoba mjini Roma, kabla ya kusafirishwa kwenda Tanzania. Moses alifariki tarehe 22 Oktoba 2009 kwenye Hospitali ya Umberto I Roma ,ambapo alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kuanguka baada ya kushuka kwenye Bus tarehe 17 Oktoba 2009. Uongozi unapenda kuwashukuru Watanzania wote waliokuja wakitokea sehemnu mbali mbali hapa Italia kama vile Napoli, Modena na Genova. Uongozi pia unatoa shukurani za dhati kwa Ubalozi wa Tanzania hapa Italy kwa kusaidia kwenye utoaji wa documentations na misaada mingine mbali mbali.
Mwili wa Marehemu Kesho 2 Novemba utasafirishwa na ndege ya KLM itakayoondoka Rome Fiumicino Airport saa mbili na dakika kumi za usiku na kufanya Transit Amsterdam kwenye mida ya saa tano asubuhi siku ya jumanne tarehe 3 Novemba. Mwili wa Marehemu unategemewa kuwasiri Julius Nyerere Airport Dar-Es-Salaam, siku ya Tarehe 3 Novembea saa tano na dakika thelathini na tano za usiku ambapo atapokelewa na ndugu zake. Mungu amlaze mahali pema Marehemu Moses Kiumbi. Amen
No comments:
Post a Comment