
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete a.k.a JK, Jana usiku tarehe 15 Nov. aliwasili Rome, Italia tayari kuudhulia Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi kuhusu hali ya Chakula Duniani ulioandaliwa na Shirika la Chakula Dunia (FAO). Kutokana na ratiba ya Mh. Raisi kuwa nzito ado haijajulikana kama Mh. Raisi atakutana na Watanzania hapa mjini Roma. Kama tutapata habari zozote tutawajulisha. Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment