Ndugu Andrew Kyabashasa wa Rome, Italy anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Mzee Godfrey Kyabulyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 17 November 2009 Katika Hospitali ya Mikocheni, Dar Es Salaam. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Burugo, Bukoba kwa ajili ya mazishi inafanyika Ada Estate Kinondoni nyumbani kwa binti yake Winifrida Kyabulyo.
Mungu alitoa, na Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe.
Kwa niaba ya Watanzania hapa Roma na Italia kwa ujumla tunakupa pole. Mwenyezi Mungu amlaze marehemu Mzee Godfrey Mahali pema peponi. Amina
Andrew Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Italia Tawi la Roma
POLE NYINGI KWA WAFIWA. MOLA AWAPE NGUVU NA SUBIRA KATIKA WAKATI HUU MGUMU. AMINA
ReplyDelete