
Juventus wanatakiwa kulipa faini ya Euro elfu 20 baada ya mashabiki wake kukutwa na tuuma za uimbaji wa nyimbo za kibaguzi zidi ya Mchezaji machachali wa Inter Mario Balotelli wakati wa mechi yake zidi ya Udinese iliyochezwa Jumapili iliyopita.
Uamuzi huu umetolewa na mahakama ya michezo ya hapa Italia baada ya mashabiki wa Juve kujiusisha na uimbaji wa nyimbo hizi za kibaguzi kwa mara nne wakati mechi inaendelea zidi ya mchezaji Balotelli ambaye anauraia wa Kitaliano lakini origini yake ni ya Ghana.
Hii inaonyesha tu ni jinsi gani mechi kati ya Juventus na Inter itakavyokuwa baada ya wiki mbili ambapo timu hizi mbili zitakutana. Itaweza kukumbukwa pia kwamba, mwaka jana pale timu hizi mbili zilipokutana kwenye Ligi hii ya Serie A, Mashabiki wa Juve walimwimbia Balotelli nyimbo za kibaguzi zikiwa na matusi ambazo ndizo zilikifanya chama cha soka nchini Italia kuweka sheria mpya ambayo inampa Refa ruhsa ya kusimamisha mpira pale ambapo kutasikika nyimbo za kibaguzi zidi ya wachezaji weusi.
No comments:
Post a Comment