

Kutokana na kuanguka kwa uchumi duniani kote, hata timu za mpira za ulaya zimejikuta zikipata matatizo kwenye ununuzi wa wachezaji na namna ya kumanage clubs hizi. Hapa Italia tumeshuudia wachezaji machachali sana kama vile Zlatan Ibrahimovic na Ricardo Kaka' wakiuzwa kwa bei za juu sana na timu za nje ya Italia, yaani Barcelona na Real Madrid. Kaka' ambaye alikuwa anategemewa kuwa Naodha wa AC Milan baada ya kustaafu Paolo Maldini, alijikuta akilazimika kuuzwa na kununuliwa na Real Madrid kwa Mamilioni ya Euro. Ibrahimovic ambaye kwenye miaka ya hivi karibuni ndiye ameiwezesha Inter kushinda ligi ya hapa (Scudeto) kwa miaka mitatu mfululizo. Kwa Mwaka huu wachezaji wengi wa Italy na makocha wameenda nje ya Italia kujaribu bahati zao maana timu za hapa zimedidimizwa sana na kuanguka kwa uchumi. Swali linakuja basi, wadamu wa Mpira wa hapa Italia mnadhani timu gani mwaka huu zitafanya vizuri kwenye Ligi na timu gani zitaanguka. na je timu hizi zitafanya vizuri kwenye Champions League au timu za England zitaendelea kusumbua maana kiuchumi angalau kidogo inaonekana wanajikongoja hivyo hivyo?
No comments:
Post a Comment