
Kongozi wa chama cha La Lega Nord, Umberto Bossi ameeleza vyombo vya habari kwamba chama chake sio cha kibaguzi. Ameeleza kwamba ni chama ambacho kina msimamo wake na unatetea msimamowake kwa meno. Amesisitiza kwamba hawana mwelekeo wowote wa kulumbana na Vatican. Bossi amesisiza kwamba kila mtu anamsimamo wake. Na msimamo wa chama chake tokea zamani haujabadilika na hautabadika hata kama unapingwa na wengi na amesema hata kama kanisa litapinga wenyewe hawataangalia nyuma. Bossi ameendelea kwa kusema kwamba, lengo la siasi ni kutengeneza sheria na kuendesha nchi na kanisa lenyewe linamalengo yake ambayo ni ya kuamsha watu na kuubiri na kuongoza watu kiroho. Ameeleza kwamba Lega Nord wapo tayari kukaachini na kuzungumza na Vatican juu ya njia mpya za maelewano na nchi zinazoendelea. Wadau kwa upande wenu hii imekaaje?
No comments:
Post a Comment