Jumuiya ya Watanzania Roma inachukua nafasi hii kuwafahamisha Watanzania wote waishio mjini Rome kuwa, kesho tarehe 25 Oktoba 2012, saa kumi kamili jioni (16hrs) pale kwenye Restaurant ya kihindi iliyopo via Principe Amedeo, kutakuwa na kikao cha dharula chenye lengo la kukusanya michango kwaajiri ya kufanikisha usafirishwaji wa mwili wa marehemu January Jeremia Mkoba kwenda nchini Tanzania kwenye pumziko la milele. Itakumbukwa kuwa marehemu Mkoba alifariki dunia mjini Napoli jumapili iliyopita tarehe 21/10/2012.
Tunaomba tujitaidi tufike mapema ili tufanikishe shughuli hii muhimu.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake liidimiwe.
Katibu,
Andrew Chole Mhella
Tunaomba tujitaidi tufike mapema ili tufanikishe shughuli hii muhimu.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake liidimiwe.
Katibu,
Andrew Chole Mhella
No comments:
Post a Comment