Jumapili 14 Oktoba , 2012 watanzania mjini Roma walipata nafasi ya kuungana na watanzania wengine wote, katika kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Chuo Cha Kipapa cha Mt. Petro, mjini Roma, kwa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu Protas Rugambwa, akishirikiana na Mwadhama Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha pamoja na Askofu Libena wa jimbo la Ifakara.
Mwadhama Kardinali Pengo
Mh. balozi Msekela akiwa kwenye meza kuu na Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Wakatoriki Roma pamoja na Mhashamu Askofu Mkuu Protas Rugambwa na Askofu Mkuu Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha.
Picha ya Pamoja baada ya Misa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma akibadilishana mawili matatu na padri.
Watanzania wengi wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. Dr. James Alex Msekela, walishiriki ibada hiyo.
Ni vema sana mnavyoishi kwa umoja na upendo
ReplyDelete