Watanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini Italy, leo walikusanyika katika Hospitali ya San Raffaele iliyopo kwenye kitongoji nje ya Roma,Monte Compatri, kwenye kuuaga mwili wa marehemu Sultan Mohamed "Domingo" aliyefariki tarehe 2 Julai 2012 akiwa kwenye matibabu ya saratani ya mapafu. Maandalizi ya kuusafirisha mwili wa marehemu yapo ukingoni na panapo majaliwa mwanzoni mwa wiki ijayo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda nchini Tanzania ambako ndugu, jamaa na marafiki wataupokea.
.
Jeneza lenyr mwili wa marehemu likiwa kwenye chumba cha kuifadhia maiti. |
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma akiuaga mwili wa Marehemu.
Baadhi ya waombolezaji wakiuaga mwili wa marehemu.
Ili ni basi lililowaleta watanzania tokea Napoli kuja kuuaga mwili wa marehemu.
Bendela ya Tanzania ilikuwepo mbeleni mwa bus lililowaleta Watanzania tokea Napoli.
Picha zote zimepigwa na mobile phone.
all rights reserved.
No comments:
Post a Comment